Filamu hiyo ya aina yake kuhusu utengenezaji wa albamu ya Kanye West DONDA imeibuka mtandaoni leo.
Haijulikani jinsi picha hizo zilivyopatikana mtandaoni lakini katika video hiyo, Kanye alionekana akifanya kazi kwenye albamu yake ya 10 studio pamoja na , watayarishaji na washiriki mbalimbali wakiwemo Pusha T, Rick Rubin, Playboi Carti na Mike Dean.
Kwenye video hiyo kanye, alionekana akiongea kupitia simu ambapo anasema kwamba yeyote ambaye hatahudhuria tukio lililozungumzwa sana katika ukumbi wa Mercedes-Benz Superdome huko Atlanta ataondolewa kwenye albamu hiyo.
“Kila mtu ambaye hayupo hapa, ninaondoa verse zao kwa hivyo ninaondoa verse ya Jay-Z, hakuna mtu yeyote hapa, kwa bahati mbaya, hawako kwenye toleo hili,” Ye anasema.
“Everybody that’s not here, I’m taking they verses off. So I’m taking Jay-Z verse off, I’m taking—there’s anybody not here, unfortunately, they’re not on this version,” Ye says. “How do you even describe these kind of conversations bro?”