Dola ya Marekani imepanda kwa kasi wakati Donald Trump akiwa karibu kushinda kiti cha Urais katika Uchaguzi wa Marekani hali ambayo imeleta matarajio ya Wafanyabiashara kuhusu kupunguzwa kwa kodi, ongezeko la ushuru wa forodha, na mfumuko wa bei chini ya utawala wa Trump.
matokeo ya uchaguzi huu yanatarajiwa kuwa na athari kubwa kwenye uchumi wa Dunia, ambapo mpka sasa imeshuhudiwa Dola ya Marekani ikioanda kwa asilimia 1.5 dhidi ya sarafu nyingine kama pauni, euro na yen ya Japan pia thamani ya sarafu ya kidijitali Bitcoin ikivunja rekodi kwa kufikia dola 75,000, huku wengi wakitarajia kuwa Trump ataimarisha soko la sarafu za kidijitali, pia bei za hisa za Tesla zimepanda kwa asilimia 14 baada ya Elon Musk amabye ndie mmiliki wa kampuni hiyo kuelezwa na Trump kuwa atachunguza matumizi ya Serikali.
Nchini Japani, soko la hisa limepanda kwa asilimia 2.6, na nchini Australia soko liliongezeka kwa asilimia 0.8. Huko Marekani, masoko ya hisa yanatarajiwa kufunguka kwa ongezeko kubwa baada ya kufunga kwa asilimia zaidi ya 1 siku ya Jumanne.
Wachambuzi wanabashiri kuwa ongezeko hili la mfumuko wa bei litafanya Benki Kuu ya Marekani kuwa na changamoto kubwa katika kudhibiti viwango vya riba ili kulinda ukuaji wa uchumi.
Aidha Wawekezaji Duniani kote watakua wakifuatilia kwa karibu mwelekeo wa masoko ya fedha, huku maamuzi ya Benki Kuu na matarajio ya biashara yakitarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye masoko ya kimataifa.