Kikao Cha Bunge kimeendelea leo MAY 26 2015 Dodoma, ukaibuka mjadala kuhusu Bangi.. Kuna nchi zimehalalisha bangi kwa matumizi ya tiba na chakula, swali la kwanza lilikuwa la Mbunge Cristowaja Mtinda aliyetaka kujua msimamo wa Serikali kwenye hili.
“Matumizi ya bangi husababisha madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchanganyikiwa, ukatili, ukorofi.. Baadhi ya sehemu Duniani hutumia bangi kama Chakula au dawa. Msimamo wa Sheria ya Tanzania inafuata Sheria ambayo inaeleza kuwa mtu yoyote atakayejihusisha na kutumia, kuhamasisha matumizi, kusafirisha ni kosa la jinai”>>>
Swali jingine; >>>“ Katika nchi yetu kuna mikoa ambayo bangi huota bila kupandwa, mfano Njombe na Iringa, wanaitumia kama chakula, Serikali imefanya utafiti gani kuona faida za kimatibabu zinazoweza kupatikana kutokana na bangi ili itumike kama dawa”>>>
Swali lake kwenye sentensi nyingine >>> “Kuna imani kwamba bangi huongeza nguvu, Serikali inatoa elimu gani kwa hao wanaotumia kwa imani ya kuongeza nguvu?“>>> Cristowaja Mtinda.
Jibu >>> “Bangi inaota bila kupandwa lakini inang’olewa na watu… Bangi ni haramu inafanya mtu achanganyikiwe na sidhani kama Serikali inaweza kuruhusu itumike.. umezungumzia kwamba bangi inaongeza nguvu sijui ni nguvu zipi za kike au za kiume”>>> Juma Nkamia.
Spika Anne Makinda akafunga hivi mjadala>>> “Tunaendelea… habari za bangi tuachane nazo”>>>
Iko kwenye sauti hii hapa, ukiplay utasikiliza stori yote toka Bungeni Dodoma.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.