Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amedokeza uwezekano wa kumpa Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla na SpaceX Elon Musk nafasi kubwa katika utawala wake iwapo atapata muhula wa pili katika Ikulu ya White House.
Katika mahojiano na Reuters mnamo Jumatatu (Ago 19), Trump alisema ana nia ya kumleta Musk katika timu yake, iwe katika jukumu la Baraza la Mawaziri au kama mshauri.
“Ningemvuta Musk kwa nafasi kama hiyo ikiwa atafanya hivyo,” Trump aliambia Reuters baada ya hafla ya kampeni huko York, Pennsylvania.
Elon Musk alijibu ofa ya Trump kwenye mtandao wake wa kijamii wa X.kuwa yupo tayari kuhudumu kwenye nafasi hiyo.