Rais wa zamani Donald Trump ameshtakiwa kwa kuhifadhi mamia ya nyaraka za siri, zikiwemo zile zilizo na siri za nyuklia za Marekani na mipango ya kijeshi.
Mashtaka ya 37 yanamshutumu kwa kuhifadhi nyaraka hizo katikanyumba yake ya Florida, ikiwa ni pamoja na katika chumba cha mpira na bafuni, na kuwadanganya wachunguzi hajui zilipo.
Inadaiwa kwamba alijaribu kuzuia uchunguzi wa utunzaji wa hati hizo.
Siku ya Alhamisi, Donald Trump alitangaza kwamba anashtakiwa na vyombo vya sheria vya shirikisho kwa usimamizi wake wa kumbukumbu za Ikulu ya White House, ikia ni kwa mara ya kwanza kwa rais wa zamani, na kwamba ameitiswa mahakamani huko Miami siku ya jumanne.
Trump, ambaye anawania tena urais 2024, amekanusha kufanya makosa yoyote.