Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump, anatarajiwa kufika Mahakamani jijini New York hivi leo kusomewa mashtaka, na kuchukuliwa alama za vidole, baada ya wiki iliyopita kustakiwa kwa kosa la kumlipa fedha mwingizaji wa filamu za watu wazima mwaka 2016.
Trump anatarajiwa Mahakamani, kusikiliza mashtaka dhidi yake, ambayo anatarajiwa kuyakataa.
Anadaiwa kumlipa mwingizaji huyo Stormy Daniels Dola 130,000 ili kukaa kimya, siku chake tu kabla ya kushinda uchaguzi wa urais.
Trump na wafuasi wake kwenye chama cha Republican, wanasema hii ni kesi ya kisiasa, kumnyamazisha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao, ambao amesema anataka kuwania urais mwaka ujao.
Trump, anakuwa rais wa kwanza wa Marekani ambaye amewahi kuongoza nchi hiyo, kufunguliwa mashtaka Mahakamani.
Ulinzi umeimarishwa katika eneo la Manhattan, ambako anapelekwa, na inahofiwa kuwa huenda kukazuka maandamano ya wafuasi wa Trump ambao wameghabishwa na kiongozi huyo wa zamani kufunguliwa mashataka.
Hati ya mashtaka inatarajiwa kufunguliwa Jumanne, na kutoa umma – na timu ya wanasheria wa Trump – maelezo ya kwanza kuhusu mashtaka maalum.
CNN imeripoti kuwa Trump atakabiliwa na mashtaka zaidi ya 30 yanayohusiana na ulaghai wa biashara kama sehemu ya uchunguzi wa malipo ya kimyakimya yaliyotolewa kwa mwigizaji wa filamu watu wazima mnamo 2016.
Timu ya wanasheria wa Trump imesema rais huyo wa zamani atakana hatia na kupinga “kila suala linalowezekana” mara baada ya mashtaka kufutwa.
Trump, ambaye ameapa kuendelea na ombi lake la 2024 licha ya mashtaka, anatarajiwa kurejea Florida baada ya kufikishwa mahakamani na kuzungumza usiku wa leo huko Mar-a-Lago.