Dozi za Chanjo ya Oxford/AstraZeneca 72,000 zilizorudishwa kwa Mpango wa COVAX na Sudan Kusini zinatarajiwa kupokelewa Kenya. Taifa hilo limezirudisha baada ya kushindwa kuzigawa kwa wakati kabla muda wake wa matumizi haujaisha.
Sudan Kusini ilipokea Chanjo 132,000 mwezi Machi lakini imefanikiwa kutoa Chanjo 8,000 tu mpaka sasa. Tayari Kenya imekamilisha taratibu zote kuzipokea.
Kenya imetangaza kubakiwa na dozi chini ya 100,000 za chanjo hiyo huku Wananchi wengi wakiwa na wasiwasi kutokana na kutopokea chanjo kwa mara ya pili.
“MAWAZIRI NI MARUFUKU KUNYANYASA WATU, KUNA WENGINE MABINGWA KUWEKA WATU NDANI”-JERRY SILAA