Inawezekana hujawahi kujua kwamba kuna watu wana macho ya rangi tofauti na ya brown, yaani kusikia mtu ana macho ya blue, au hata kuhisi kwamba inawezekana kwamba rangi ya macho ya watu ikatofautiana.
Inaaminika kuwa watu wenye macho ya blue ni wazungu tu tena wa asili ya caucasus ambao wanapatikana katika mipaka ya bara la Ulaya na bara la Asia katika maeneo mengi ya Urusi, Georgia, Azarbaijan, na Armenia pamoja na baadhi ya maeneo ya Uturuki.
Ukweli ni kwamba suala la mtu kuwa na macho ya blue, sio suala la rangi ya ngozi ya mtu husika bali ni suala la vinasaba yaani genes.
Mwaka 2008, timu ya wanasayansi wa nchini Denmark wa Chuo Kikuu cha Copenhagen wakiongozwa na Professor Hans Eiberg wa chuo hicho walieleza kuwa miaka mingi sana ya nyuma, kila binadamu duniani alikuwa na macho ya rangi ya brown.
Takribani Miaka 10,000 iliyopita kwa mara ya kwanza alizaliwa mtu ambaye alikuwa na macho ya mwanga yaani macho yaliyokuwa yana rangi kama nyeupe, tofauti kabisa na watu wengine.
Rangi ya macho ilianza kubalidilika kutoka rangi ya brown, baada ya mabadiliko yaliyotokea na kuathiri kinasaba cha OCA2 ambacho ndicho kilikuwa kikitengeneza rangi ya brown ya jicho.
Mabadiliko hayo yalipelekea kutengenezwa kwa switch ambayo ilizima uwezo wa kutengenezwa kwa rangi ya brow ya jicho kama ilivyokuwa hapo awali na huo ukawa mwanzo wa kuzaliwa baadhi ya watu ambao walikuwa na macho ya rangi nyingine kama blue na kijani hadi leo.
‘Tunatengeneza Barabara baada ya Miezi mashimo yanatokea Tunaanza kulaumiwa’ Benjamini Sitta