Staa wa kimataifa wa Chile anayeichezea Arsenal ya England Alex Sanchez ni miongoni mwa wachezaji wa Arsenal ambao wamegoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia club hiyo lakini wengi wamekuwa wakitaja kuwa anaweza akauzwa January.
Sanchez mkataba wake na Arsenal una malizika mwisho wa msimu wa 2017/2018 hivyo hadi dirisha la usajili la kiangazi kama hatokuwa ameamua kuongeza mkataba ataondoka kama mchezaji huru, hivyo kocha wa Arsenal Arsene Wenger ambaye amekiri kutokuwa tayari kumuuza amesema itawagharimu.
Wenger ambaye hataki kumuachia Sanchez aondoke Arsenal katika kipindi cha usajili kutokana na umuhimu wake, anaamini kuwa kuondoka kwa staa huyo mwishoni mwa msimu kutawagharimu Arsenal pound milioni 70 au zaidi ili kupata mbadala wake, pound milioni 70 ni zaidi ya Tsh bilioni 200.
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0