Club ya Stade Reims ya Ligi Kuu nchini Ufaransa imethibitisha kifo cha doctor wa timu yao Bernard Gonzalez ikiwa ni siku chache zimepita toka athibitike kuwa ana virusi vya corona.
Dr Gonzalez amefariki sio kwa corona ila aliamua kujiua mwenyewe baada ya kujua kuwa amepata maambukizi ya virusi vya corona, Gonzalez ,60, ameacha barua ya kueleza sababu ya kujiua kwake.
Bernard Gonzalez amekuwa Dr wa club ya Stade Reims kwa miaka 20, Meya wa Reims Mr Arnaud Robinet ameeleza kusikitishwa kwake juu ya kifo hicho na kuwapa pole familia.
”(Gonzalez) alikuwa ni Dr wa club na mwanataalum mweledi alikuwa anatambulika na kukubalika kwa wote, natoa pole kwa wazazi, mkewe na familia yake”>>> Arnaud Robinet