Dr. Dre na Angie Martinez ni miongoni mwa wataalamu 31 wa burudani ambao wamechaguliwa tuzo ya Hollywood Walk of Fame inayotamaniwa na wengi.
Siku ya Jumatatu (Juni 26), kamati rasmi ya uteuzi ya Walk of Fame iliyojumuisha washindi wa zamani wa Walk of Fame ilitangaza washindi wapya katika mkutano na waandishi wa habari na walichagua washindi wapya kutoka miongoni mwa mamia ya uteuzi.
Ellen K, mtangazaji maarufu wa redio ya KOST na mwenyekiti wa kamati ya uteuzi ya Walk of Fame, alitangaza washindi wapya katika mkutano na waandishi wa habari mnamo Jumatatu Juni 26, ambao ulirushwa moja kwa moja The Aster huko Hollywood.
“Kamati ilifanya kazi ya kubwa kuchagua watu hawa wenye talanta,” alisema. “Hatuwezi kusubiri kuona majibu ya kila mtu kama wanatambua kwamba wanakuwa sehemu ya historia ya Hollywood’
“The committee did an amazing job choosing these very talented people,” she said. “We can’t wait to see each honoree’s reaction as they realize that they are becoming a part of Hollywood’s history with the unveiling of their star on the world’s most famous walkway!”
Dre na Angie, Toni Braxton, Otis Redding, na mwigizaji wa Abbott Elementary Sheryl Lee Ralph walikuwa miongoni mwa waliochaguliwa kwenye tuzo hiyo.
Haikutajwa tarehe husika au nyakati zilizopangwa kufanyika kwa sherehe hizo.
The Walk of Fame ilianzishwa mwaka wa 1960, na ina zaidi ya nyota 2,700 huko Los Angeles.
Katika mahojiano na Billboard mwezi Mei, Ana Martinez, mtayarishaji wa sherehe za Walk of Fame, alibainisha kuwa pamoja na kuwa kivutio cha watalii maarufu duniani, jina hilo ni heshima ya hali ya juu.