Wanajeshi wasiopungua 22 wamehukumiwa kifo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mahakama ya kijeshi ya Butembo, iliyokkutana katika kesi ya wazi ya Lubero, kaskazini mwa mkoa wa Kivu Kaskazini, imewapata wanajeshi hao na hatia ya “uoga, kuharibu silaha za kivita na uporaji”.
Hii ni hukumu mpya ya kifo mashariki mwa DRC katika mazingira ya mvutano kutokana na kusonga mbele kwa waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.
Hukumu hiyo ilitolewa mapema alasiri ya Jumatatu Julai 8. Wanajeshi 22 wa vikosi cha vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) walihukumiwa kifo, baada ya siku nne za kusikilizwa mbele ya mahakama ya kijeshi iliyokutana katika mahakama huko Lubero, haswa kwa kuwakimbia waasi wa M23.
Hukumu hii itakuwa kama mfano na inapaswa kuwahimiza watu kuwashutumu askari wanaofanya unyanyasaji dhidi ya raia.
“Tumewaambia hata raia: mkiona kuna askari wanakiuka sheria, msikose kutoa taarifa kwa ofisi ya mwendesha mashtaka. Hatutasita kuchukua hatua kuwazuia wasiendelee na vitendo vyao. Iwe ni mimi au raia, tumeridhika,” alisema Kapteni Kahumbu Muhasa Mélissa, naibu wa kwanza wa mwendesha mashitaka katika mahakama ya kijeshi ya Butembo.