Chama cha UDPS cha kwake rais Felix Tshisekedi kimeshinda vita 66 vya ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita, kikiwa ni chama kinachoongoza katika kura hizo.
Matokeo hayo yaliyotangazwa siku ya Jumapili, yanaonesha kuwa chama chake Tshisekedi kimevishinda vyama vingine kwa nafasi 44, idadi hiyo ya wabunge 66 ikiwa imepanda kwa nafasi 25 ikilinganishwa na uchaguzi wa 2018.
Idadi hii inampa rais Tshisekedi mamlaka kuongoza muungano tawala wa Sacred Union na kuunda serikali mpya.
Vyama tanzu vinavyomuunga mkono vinavyoongoza na washirika wake kama spika wa bunge; Modeste Bahati Lukwebo, waziri wa ulinzi Jean Pierre Bemba na waziri wa uchumi Vital Kamerhe vilishinda viti 35, 17 na 32 kila moja.
Matokeo hayo yametangazwa huku upinzani na sehemu ya waangalizi wakiendelea kuibua maswali kuhusu mchakato wa uchaguzi ulioshuhudia vurugu maeneo mengine wakati wa upigaji kura na uhesabuji.