Rais Samia Suluhu Hassan ameidhinisha zaidi ya Sh trilioni 1.4 katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wake ili kutekeleza mradi wa kufua umeme wa maji katika bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) ambao sasa umefikia asilimia 56.
Waziri wa Nishati, Januari Makamba ameiambia kamati ya bunge ya nishati na madini kwamba kasi ya utekelezaji mradi huo imeongezeka kutokana na mikakati kadhaa inayotekelezwa na serikali ikiwemo kumlipa mkandarasi kwa wakati.
MAMBO MAKUBWA MATANO ALIYOFANYA HAYATI MAGUFULI, HAYATOSAHAULIKA TANZANIA