Leo March 1, 2018 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Shein amekutana na uongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kusisitiza haja ya kuendeleza umoja na ushirikiano na Tume ya Zanzibar (ZEC) ili Tanzania iendelee kuheshimiwa.
Dkt. Shein amesema hayo akiwa katika mazungumzo na uongozi wa NEC, Ikulu mjini Zanzibar ukiongozwa na Jaji Semistocles Kaijage Mwenyekiti wa Tume hiyo akifuatana na Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid pamoja na Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani.
Dkt. Shein ameupongeza uongozi wa tume kwa kuendeleza umoja na ushirikiano uliopo kati ya (NEC) na (ZEC) huku akisisitiza haja ya kuendelezwa ili kuendelea kuijengea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuendelea kufanya kazi zao kwa ufanisi.
“Ushirikiano wa pamoja utasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza majukumu kwa Tume zote mbili hasa ikizingatiwa kuwa kila upande una uzoefu wake ambapo kwa Zanzibar masuala ya uchaguzi hasa wa vyama vingi yalianza tokea mwaka 1957 na baadae kuendelea hadi hivi leo.” -Dkt. Shein
“Nimevutiwa na mafanikio yaliopatikana na Tume kutokana na kutekeleza majukumu yao yakiwemo ya kuhakikisha wananchi wanatumia haki yao ya msingi ya kupiga kura, wanaendesha chaguzi, wanasimamia na hatimae wanatoa matokeo kwa wakati,” –Dkt. Shein
“Matumaini yangu kuwa Mwenyekiti ataendeleza majukumu yake kama alivyofanya Mwenyekiti aliyekuwa kabla yake Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ambaye muda wake wa kushika wadhifa umemaliza kwa kutoa ushirikiano mzuri na NEC” -Dkt. Shein
MAAMUZI: SIKU 100 TOKA MWANDISHI WA MWANANCHI ACHUKULIWE NA WASIOJULIKANA