Hii imetoka kwenye jiji la Mbeya ambalo linaongozwa na Amos Makalla kama Mkuu wa mkoa ambapo taarifa ya leo muhusika mkuu ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson.
Dr. Tulia ameitembelea tena Mbeya na kwa kupitia TULIA TRUST akatoa shilingi milioni 40 baada ya kuumizwa sana moyo na hali aliyoikuta miezi sita iliyopita kwenye kituo cha Afya cha Ruanda ili pesa hizo zikasaidie ujenzi wa chumba cha upasuaji, ni baada ya kujionea Watu wanavyoteseka.
Akiwa kwenye eneo la tukio alisema “Mwezi March tulifika hapa tukiwa na mbio za Tulia Marathon na tulikuja hapa ili tujenge choo lakini tukaambiwa hilo sio tatizo kubwa kama chumba cha upasuaji, leo tumekuja hapa kutimiza ahadi na Mkandarasi ameshaanza kazi”
Baada ya Mkuu wa Mkoa Amos Makalla kukabidhiwa hundi ya pesa hizo alisema yafuatayo… “Nikushukuru sana Naibu Spika kwa msaada huu mkubwa, sio wote ambao wanazo wanauwezo wa kutoa“
“Sio kwamba Dr. Tulia anazo sana na hana matatizo yakwake na familia au kusaidia ndugu zake lakini ametafuta hizi fedha aje aokoe maisha ya kina mama na Wananchi wa jiji la Mbeya” – Amos Makalla
Full video nimekuwekea hapa chini tayari…