Leo March 24 Kikao cha Bunge kimeendelea Dodoma ambapo Muswada wa Sheria ya Kupambana na dawa za kulevya uliwasilishwa na Wabunge walipata nafasi ya kuchangia Muswada huo.
Kangi Lugola, Yusuph Salim na David Silinde ni baadhi ya Wabunge waliochangia muswada huo; “Tatizo kubwa la kwanza kabisa waheshimiwa wabunge ni tabia ya kulindana kuwalinda wafanyabiashara ambao ndio wanafanya biashara za madawa ya kulevya, ni kweli wanafahamika kwa majina na mahali wanapoishi.
Lakini kwa sababu tumeamua kuwalinda kwa sababu na sisi tunanufaika hatutaki kuweka mamlaka wakati bado tabia hii ya kulindana tunayo tatizo la madawa ya kulevya halitaondoka katika nchi yetu, Jeshi la Polisi pale wakimkamata mfanyabiashara wa madawa ya kulevya simu za wakubwa zinapigwa wanawaacha akipelekwa mahakamani kumejaa rushwa kesi haziendi wanamuachia“– Kangi Lugola.
“Leo Wabunge tunataka kumchomekea Kangi ataje wakati waliowahi kutaja na kupambana na watu hawa hata walipopoteza maisha hawakumbukwi, Kangi Lugola tunampenda au hatumpendi jamani?“
Tunajadili vitu ambavyo uwezo wetu wa kukabiliana navyo unaonekana dhahiri ni mdogo tunavyozungumzia dawa za kulevya tunazungumzia sehemu yenye watu wenye nguvu watu wenye fedha watu wenye uwezo wa kumfanyia mtu kitu chochote na wasifanywe chochote“
“Vyombo vya habari ushauri wangu visingetaja thamani ya madawa.. ni bora vingetaja athari lakini vikataja na adhabu anayotakiwa kupewa. Ukiitangaza ile adhabu kwamba madawa aliyokutwa nayo adhabu yake ni kunyongwa mpaka kufa wote watakaoiona hiyo taarifa halafu wakaona asubuhi kanyongwa watu wataogopa…”–Mbunge Livingstone Lusinde.
“Uangalie tena sasa familia ya yule kijana ambae anatumia madawa ya kulevya namna ambavyo imeathirika kiuchumi imefilisika kwa sababu vijana wale wanaadhiri familia zao wanaharibu kila kitu ndani za familia zao“
Wakati mwingine wanaiba mpaka vikombe ili auze apate unga, athari ambayo mtu mwenyewe anapata, athari ambayo familia ya kijana mla unga anaipata kwa sababu tu ya tamaa ya mtu mmoja au wawili halafu Serikali inawafumbia macho watu hawa kwakweli ni kitu ambacho kinasikitisha sana nakubaliana kwamba Serikali nayo inashiriki“ — Mbunge Yusuph Salim.
“Wanaofanya biashara ya dawa za kulevya sio wauza ndizi wala sio mtu mwenye mtaji wa milioni tano wala kumi ni watu wenye hela nyingi, ndio maana hapa kila mmoja anasema ana majina halafu anatetemeka kuwataja sababu anajua akitoka tu hapa kichwa chake ni halali yao.
“Hivyo ndivyo ilivyo na alipokuwa anamalizia Kangi Lugola, akawa anasema anaweza kuwataja hao watu ila hofu yani ni kuna watu kulekule ndani anapowataja wanatoa siri kwamba aliyetuletea haya majina ni Kangi Lugola.. hiyo ndio hofu iliyopo maana yake ni kwamba Serikali inashindwa kuwalinda wale wanaoleta hizo siri“–Mbunge David Silinde.
Bonyeza play kuwasikiliza Wabunge hao;
1. Mbunge David Silinde
2. Mbunge Kangi Lugola
3. Mbunge Livingstone Lusinde
4. Mbunge Yusuph Salim
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook