Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Kituo cha utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) wako mbioni kukamilisha utafiti wa mbegu ya mahindi iliyowekwa vinasaba vyenye uwezo wa kukinzana na wadudu waharibifu aina ya viwavi jeshi vamizi wa mahindi ambao hawana dawa na kwa muda mrefu wamekuwa kikwazo kwa wakulima wengi nchini.
Utafiti huo unaofanyika katika kituo cha utafiti wa kilimo Makutupora mkoani Dodoma umefikia asilimia 80 ya lengo na tayari umeonyesha ufanisi wa hali ya juu ikilinganishwa na mbegu chotara za kawaida ambazo hutumiwa na wakulima wengi nchini .
Kilio cha wanafunzi BUKOBA Baada ya kuhamishiwa Shule nyingine