Ni Habari kutoka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam leo November 28 2017 ambayo imetoa hukumu ya miaka 10 jela kwa Mfanyabiashara wa Dar es salaam.
Mfanyabiashara aliehukumiwa ni Gairo Mtozoma ambae umri wake ni miaka 43, kilichofanya ahukumiwa miaka yote hiyo kumi ni kukutwa na makosa mawili ya kupatikana na silaha pamoja na risasi.
Mtozoma ambaye pia ni Mkazi wa Magomeni Kagera ameukumiwa kifungo hicho na Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa baada ya Wakili wa Serikali Nassoro Katuga, kueleza kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya hukumu.
Kabla ya hukumu hiyo, Katuga aliiomba Mahakama itoe adhabu kwa Mshitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine, kwenye hii video hapa chini utaweza kumuona Mfanyabiashara mwenyewe.
Mchungaji auliwa na Mgonjwa mwenye mapepo Morogoro, bonyeza play hapa chini kuipata hii
EXCLUSIVE VIDEO: MILIONEA SUMRY HATAKI TENA KUSIKIA BIASHARA YA MABASI, ATUONYESHA ALIKOJICHIMBIA…. BONYEZA PLAY HAPA CHINI