Serikali ya Kenya inajikuta inapandishwa tena Mahakamani ndani ya kipindi cha wiki mbili mfululizo kwa kukiuka agizo la Mahakama la kuvifungulia vyombo vya television ilivyovifungia wiki iliyopita vya Citizen TV, Inooro TV, KTN News na NTV baada ya kupewa kurusha matangazo ya ‘kujiapisha’ kwa Kiongozi wa Upinzani NASA Raila Odinga.
Mashtaka hayo yamefunguliwa na Mwananharakati Okiya Omtata leo February 5, 2018 na kuomba Mahakama izitaje mamlaka na watu maalum ambao wamedharau agizo hilo la Mahakama huku akifungua mashtaka hayo kwa hati ya dharura ili yashughulikiwe haraka.
Jaji wa Mahakama ya Juu nchini humo Chacha Mwita Ijumaa ya wiki iliyopita alitoa maelekezo kwa Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo kuvifungulia vituo hivyo vya television ambavyo vilizimwa January 30, 2018.
Kilichozungumzwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu wake na Majaji baada ya kuapishwa na JPM