Leo November 17, 2017 Benki ya Diamond Trust Tanzania LTD imeitambulisha rasmi Account maalum kwa asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali iitwayo DTB COMMUNITY ACCOUNT isiyo na makato yoyote wala gharama za uendeshaji ikiwa na lengo la kufikia watu wengi zaidi kupata huduma za kibenki.
Akaunti hiyo ya DTB Community inafunguliwa kwa shilingi ya Kitanzania (TSHS) au dola ya Kimarekani (USD) na mteja anapata fursa ya kufanya miamala kupitia mtandao kwa saa 24 kwa siku na pia atapata faida kila mwezi ikiwa atakuwa na salio la shilingi milioni 50 au dola za kimarekani elfu hamsini (USD 50,000) ikiwa ni pamoja na kupata huduma ya malipo ya mishahara ya wafanyakazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa DTB Tanzania, Ng. Viju Cherian alisema “kimkakati, lengo letu ni kuwa na huduma kwa ajili ya Watanzanian wote bila kujali rika, jinsia au kipato.”