Upo msemo unaosema umri ni namba tu na hii inadhihirika pindi tunaposhuhudia watu wanafanya mambo mbalimbali ambayo kwa tafsiri ya jamii huwa yako tofauti kabisa na umri wao. Kwa kuzingatia hilo wafuatao ni wanawake wazee 6 wenye miaka zaidi ya 60 ambao mpaka leo bado ni wanamitindo na bado wanafanya kazi yao vizuri.
7. Maye Musk (miaka 69)
Huyu ni mama mzazi wa Elon Musk ambaye ni mwekezaji, na mjasiriamali mkubwa duniani. Maye alianza uanamitindo tangu ana umri wa miaka 15 akiwa Afrika Kusini ambako alizaliwa na kukua huko.
6. Veruschka von Lehndorff (miaka 77)
Huyu ni mwanamitindo ambaye ana asili ya nchini Ujerumani ambaye alikua na umaarufu mkubwa sana miaka ya 1990. Bado anashirikiwa katika picha za majarida mbalimbali hadi leo.
5. Carmen Dell’Orefice (miaka 85)
Anaelezwa kuwa kwenye tasnia ya mitindo kwa miaka takriban 70 na alitokea kwenye cover ya jarida la Vogue akiwa na umri wa miaka 15.
Akiwa anaelekea miaka 30 ya umri wake alistaafu kazi hiyo na kurudi tena mnamo miaka ya 70 na kuendelea kufanya uanamitindo hadi sasa.
4. China Machado (miaka 86)
Alizaliwa na kukua jijini Shanghai nchini China kabla ya kuondoka nchini humo na familia yake kuelekea New York baada ya Japan kuvamia nchi yao mnamo 1937. Amefanya kazi nyingi za uanamitindo, ikiwa ni pamoja na kutokea kwenye majarida mbalimbali.
3. Baddie Winkle (miaka 88)
Mwanamitindo huyu mwenye miaka 87 sio tu star wa mitindo bali pia anatajwa kuwa mpenzi mkubwa wa mitandao ya kijamii.
2. Daphne Selfe (miaka 88)
Nyota yake ilianza kung’ara pindi aliposhiriki kwenye usaili wa kushirikishwa kwenye jarida la London magazine akiwa na umri wa miaka 20 mnamo mwaka 1949. Baada ya hapo alianza kazi yake hiyo rasmi na alitokea kwenye majarida mengine mbalimbali. Mwaka 2015 alipewa tuzo na kuingizwa kwenye kitabu cha dunia cha kumbukumbu yaani ‘Guinness World Record’ kama mwanamitindo mzee kuliko wote duniani ambaye bado anaendelea kufanya kazi.
1. Bo Gilbert (miaka 101)
Huyu ndiye mwanamitindo mzee kuliko wote duniani. Mwaka jana wakati Vogue inatimiza miaka 100 walimtumia yeye kuwa model wa cover ya jarida hilo.
Ulipitwa na hii? FASHION: Ni mwanamitindo mpya ametuleta haya mavazi ”Kimono”