Kutoka nchini Kenya, leo March 2, 2018, ni kuhusu madaktari wa Hospitali ya Kenyatta wamefukuzwa kazi huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufuatia kufanya upasuaji wa kichwa kwa mtu ambaye hakutakiwa kufanyiwa upasuaji huo.
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Lily Tare, amevieleza vyombo vya habari ya kuwa kulikuwa na wagonjwa wawili, mmoja ndiye aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa kwani alikuwa na damu iliyovimba ndani ya kichwa.
Tare ameeleza kuwa waliohusika na kwa sasa tayari wanafanyiwa uchunguzi kupitia sakata hilo ambao ni daktari wa upasuaji wa ubongo, muuguzi, na mtalaamu wa dawa za usingizi.
Hatahivyo ameomba radhi na kueleza kuwa mgonjwa halisi aliyekuwa anatakiwa kupasuliwa kichwa tayari ameshafanyiwa upasuaji huo na afya yake tayari imeanza kuimarika.
LIVE: Sababu za Viongozi wa ACT Wazalendo kuhamia CCM
BREAKING: Baadhi ya Viongozi wa ACT Wazalendo wahamia CCM