Afya ni kitu cha msingi sana katika maisha ya kila binadamu. Hata hivyo afya njema ni mchanganyiko wa vitu mbalimbali ambavyo vinaujenga na kuulinda mwili. Vitu hivyo ni kama vyakula, vinywaji, mazoezi na vinginevyo.
Leo January 24, 2018 Ayo TV na millardayo.com inakuletea vyakula vitano ambavyo vitasaidia ngozi yako kuwa na afya pamoja na kuwa na muonekano mzuri kama wa mtoto kwa kadri mtu anavyoendelea kukua.
Wine Nyekundu
Wataalamu mbalimbali wa masuala ya afya wanaeleza kuwa mvinyo una manufaa mengi kwa afya ikiwa ni pamoja na kupunguza hatari ya kifo cha mapema kwa mara tano.
Inaelezwa kuwa resveratrol ambayo inapatikana katika ganda la zabibu ambalo ndilo tunda kuu la kutengenezea mvinyo mwekundu yaani ‘red wine’ huwa na virutubisho ambavyo hufanya ngozi isizeeke.
Maboga
Inaelezwa kuwa maboga huwa na utajiri wa Beta-carotene Vitamini A, E na C. Virutubisho hivi husaidia kupunguza kasi ya mwili kuzeeka na kuzuia makunyazi ya ngozi. Hii inamaanisha kuwa ngozi huwa kama ya mtoto pindi mtu anapoendelea kukua.
Chocolate nyeusi
Hizi ni zile zenye rangi ya kahawia iliyokolea maarufu kama dark chocolate. Wataalamu mbalimbali wanaeleza madhara ya kula chocolate nyingi ikiwa ni pamoja na kuongezeka uzito wa mwili.
Hata hivyo inaelezwa kuwa chocolate nyeusi ukilinganisha na nyeupe huwa na kirutubisho kinachoitwa flavanols ambacho hukinga ngozi dhidi ya mionzi ya jua na hata kusaidia kurudisha kumbukumbu zinazopotea kutokana na uzee au kuongezeka umri.
Mafuta ya mzeituni (Olive Oil)
Mafuta haya yanatajwa kuwa na manufaa makubwa sana kwenye mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kuweka ngozi kwenye hali ya kutozeeka mapema.
Marufuku kuanzia leo Mama kubeba Mtoto na kwenda nae sokoni Arusha
Sheria inasemaje kwa alichofanya Nabii Tito ???