Dua Lipa amezua gumzo za shangwe kwenye sherehe ya Krismasi baada ya kutangaza kuwa amechumbiwa
Mwimbaji huyo wa Radical Optimism alienda kwenye Instagram yake kuonesha pete yake ya uchumba .
Akichapisha picha yake akiwa amevalia suruali nyeupe yenye Lipa aliandika kwenye nukuu, “Krismasi ilikuwa nzuri sana.
Mashabiki walifurika sehemu ya maoni ili kushiriki maoni yao ya kushtushwa na chapisho la Dua, linaloangazia pete yake kubwa.
Hivi sasa ndoa inanukia kwa mwanadada Dua Lipa.
Mwimbaji huyo wa Kialbania mwenye umri wa miaka 29, ambaye amekuwa akihusishwa kimapenzi na mwigizaji Callum Turner, aligonga vichwa vya habari mapema mwaka huu baada ya kuonekana pamoja kwa mara ya kwanza Januari katika tafrija ya Masters of the Air huko London.