Moja ya story ambayo imechukua sehemu kubwa ya habari kwenye vyombo vya Kimataifa ni hii ishu ya moto mkubwa ambao umeteketeza sehemu kubwa ya ghorofa usiku wa kuamkia leo February 21 Dubai.
Kilichofanya habari hii kuchukua nafasi kubwa ni kwamba ghorofa hili liko kwenye rekodi ya maghorofa marefu zaidi DUNIANI.
Ghorofa liko mtaa wa Marina, liliwaka moto saa nane usiku kwa saa za Dubai, hakuna ripoti ya vifo vya watu, kutokana na urefu wa ghorofa hata watu waliokuwa kwenye majengo ya jirani nao walijikuta wakikimbia kujiepusha na balaa lolote ambalo lingeweza kuwakuta, kilichowatia hofu zaidi ni cheche nyingi ambazo ziliruka sehemu kubwa kuzunguka jengo hilo.
Rekodi zinaonesha hili lilikuwa ghorofa refu duniani ambalo ni kwa ajili ya apartments ambazo walikuwa wakiishi watu zaidi ya 600 ambao asilimia kubwa yao walitoka salama, watu wanne walitoka wakiwa na majeraha madogo.
Mashuhuda wanasema jengo hilo lina alarm ambazo zingelia kutoa tahadhari ya moto lakini hazikufanya kazi, watu wa maghorofa ya jirani walitoa taarifa kwa Zimamoto baada ya kuona moto huo unawaka.
Vikosi vya Zimamoto viliweza kuudhibiti moto huo muda mfupi baadaye, chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.
Hii ni video iliyorekodiwa wakati wa tukio hilo.