Pamoja na mji wa Dubai kufahamika kwa mashopping ya bei ghali na anasa za kila aina, bado kuna vitu ambavyo unaweza kufanya bila ya kutumia pesa yeyote ile wala kulipa kiingilio, Acha nikusanue.
PALM FOUNTAIN JUMEIRAH:
Hii ni sehemu ambayo unaweza kutazama maji yakiwa yanacheza, sehemu hii kuna njia mbili juu ya maji na taa za LED 3000 ambazo zinamulika maji haya pale ambapo yanaruka juu kupitia njia zake.
Maji haya huwa yanaruka na kucheza muziki wa wasanii tofauti tofauti duniani na show hii huwa inaanza baada ya jua kuzama, mpaka usiku.
ALSERKAL AVENUE
hii ni kwa mashabiki wa magari, hapa unaweza kuona magari ya kila aina ya dunia, BMW, Ferrari,Porsche utake wewe tu! Magari haya ni ya viwango vya juu, ya kizamani, ya kisasa, ya kihistoria na zaidi.
Makumbusho ya U.A.E
Hapa unapata nafasi ya kuona vitu vingi vya kumbukumbu kuhusu historia ya Dubai kabla ya kuanza kubadilishwa mwaka 1996, itakushangaza kuona jinsi jangwa lilivyotengenezwa kuwa mji ambao ni kivutio kikubwa hivi sasa duniani na nyumba ya technolojia, Makumbusho hii inapatikana maeneo ya Deira pale Souk Al Marfa.
MUSEUM OF THE FUTURE
Ukipita barabara ya Sheikh Zayeed road ni hakika utapishana na jengo la Makumbusho ya siku za mbeleni kwa Dubai (Museum of the future) jengo hili ni la kuvutia kwa namna lilivyojengwa na ni moja kati ya vivutio vikubwa.
Humo ndani kuna teknolojia za kila namna zilizotengenezwa na wahandisi wajao Dubai wa kila aina, kila mwenye utaalamu wake mtaani ameuweka humo, na hivyo watalii hupita kutazama siku za mbeleni za Dubai zitakuaje kwa mujibi wa teknolojia walizozitengeneza.
Dubai Aquarium and Underwater zoo:
Ukitembelea mall ya Dubai Mall ndani yake utakutana na bwawa kubwa la samaki lililojengwa, bwawa hili limejaa aina nyingi za samaki wapatikanao duniani, na kuingia Dubai Mall ni bure kabisa.