Mshambulizi wa Aston Villa Jhon Duran amesaini mkataba mpya na klabu hiyo hadi 2030.
Durán, 20, amefurahia msimu mzuri sana akiwa Villa Park msimu huu, akifunga mabao sita, likiwemo la ushindi dhidi ya Bayern Munich Jumatano kwenye Ligi ya Mabingwa.
Ametumiwa sana kama mchezaji wa akiba, lakini mara tatu kwenye Ligi Kuu msimu huu amefunga bao la ushindi kwa upande wa Unai Emery.