Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni leo February 23, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari ameeleza kuwa kuanzia March 1, 2018 Kikosi cha Usalama Barabarani kitaanza rasmi ukaguzi wa magari ya watu binafsi nchini nzima kwa kipindi cha miezi miwili.
Ameeleza kuwa kwenye ukaguzi huu, itafanyika tathmini ya kuona kama magari hayo yanafaa kutembea barabarani na watapewa sticker maalumu na kulipa kiwango cha Tsh 3000.
Ameeleza kuwa tathmini iliyofanywa siku za hivi karibuni na Kikosi cha Usalama barabarani imebaini upungufu wa ajali barabarani ambapo kwa kipindi cha July hadi December 2017 walifanikiwa kupunguza ajali zilizosababisha vifo 1330, majeruhi 2748.
Ukilinganisha na kipindi hicho hicho kwa mwaka 2016, ajali zilizotokea zilikuwa 2704, na kusababisha vifo 1676 na majeruhi 2499, haya ni mafanikio ya kupunguza ajali kwa kiwango cha 43% kutoka 10%.