Leo January 23, 2018 Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limethibitisha kumkamata Tito Onesmo Machibya ambaye anajiita ‘Nabii Tito’ ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nong’ona kilicho nyuma ya Chuo Kikuu cha Dodoma.
Kamanda wa Polisi Dodoma Gilles Muroto ameeleza kuwa January 16, 2018 mtuhumiwa huyo alikamatwa na Jeshi hilo la Polisi akituhumiwa kurusha vipande vya matangazo ya video na picha vyenye maudhui ya kukashfu dini nyingine na kuleta chuki dhidi ya watu wengine.
“Kijana huyu ameonekana akirusha kwenye mitandao ya kijamii na kusambaza vipeperushi kwenye maeneo ya starehe, kutangaza dini inayokiuka maadili ya nchi hadharani na kufanya vitendo ambavyo havifai na kutumia kitabu cha Biblia ambacho hafungamani nacho.” – Kamanda Mroto
LIVE: Jeshi la Polisi Kinondoni wazungumza kuelekea uchaguzi mdogo Feb 17