Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Jeshi la Zima Moto wametia saini makubaliano (Memorandum of Understanding) ambayo wamekubaliana mambo kadhaa yenye lengo la kukuza uhusiano baina yao ili kuongeza ushirikiano na ufanisi katika kazi.
Moja ya malengo ya makubaliano hayo ni kutoa mafunzo kwa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji kutokana na kwamba uhaba wa mafunzo imekuwa moja kati ya hoja kubwa za ukaguzi kila viwanja vya ndege vinapokaguliwa na mashirika ya ukaguzi duniani.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Richard Mayongela amesema kwa kuanza kutekeleza lengo hilo, mwezi huu wa February Mamlaka hiyo itatoa Tsh Milioni 120 kwa ajili ya mafunzo ya Jeshi la Zima Moto.
“Wengi kwenye haya maeneo ya kazi hawajapata mafunzo, na wengine wamepata muda mrefu sana umepita na mambo ya uzimaji moto katika viwanja vya ndege yanabadilika mara kwa mara hivyo ni lazima wawepo Askari ambao wanamafunzo stahiki na vifaa vya kisasa ili kutatua changamoto mbalimbali zinazotokea katika viwanja vya ndege.” – Richard Mayongela
Watoto waliokutwa Sokoni Arusha wamekamatwa, Wazazi wajitokeza