April 11 2016 Serikali ilitoa zabuni kwa JKT kutengeneza madawati 60,000 kwa gharama ya Bilioni 3 ambapo bei ya kila dawati ni sh 50,000/, aidha July 13 2016 JKT ilikabidhi madawati 32,387.
Leo August 23 2016 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi amekutana na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa katika awamu ya pili madawati 20,000 yameshakamilika na yanaweza kuchukuliwa kuanzia sasa kwenda kwenye majimbo yaliyopangiwa kupata madawati hayo.
Katika kutekeleza mpango huo, awamu ya kwanza jumla ya madawati 32,387 yalitengenezwa na yaliyochukuliwa na Wabunge kwa kushirikiana na Halmashauri zao ni 22,721 tu, hivyo madawati 9,666 sawa na asilimia 30% bado hayajachukuliwa na Majimbo husika.
Akizungumzia Majimbo ambayo hayajachukua madawati yake katika awamu ya kwanza Dkt. Mwinyi amesema ni vyema Viongozi katika Majimbo hayo wakiwemo wabunge wanatakiwa wakachukue madawati hayo ndani ya siku 7 ambapo mwisho itakuwa August 30 2016
Majimbo ambayo hayajachukua madawati yake katika awamu ya kwanza yametajwa kuwa ni Kilindi, Pangani, Makambako, Ludewa, Wangingombe na Makete. Majimbo mengine ni Kyela, Rungwe, Busokelo, Songwe, Kwela, Tunduru, Iringa Mjini, Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini na Ileje Nkasi Kaskazini na Nkasi Kusini.
ULIKOSA MANENO YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KWA WANAOTAKA KUANDAMANA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI