Mbunge wa Kigoma Kusini Hasna Mwilima ameilalamikia Serikali ikiwemo idara ya uhamiaji kuacha uonevu kwa watu wa Kigoma kwa kusema wao sio wananchi wa Tanzania na wakati mwingine kuwavamia katika nyumba zao usiku ili wawakague uraia wao.
“Tuna kero kubwa sana na uhamiaji ndani ya mkoa wa Kigoma, leo hii watu wa Kigoma hatuna amani tunaitwa Wakongo, warudi… roho inatuuma. Unaposikia watu wanavamiwa saa nane za usiku ile kigoma ni Tanzania.” –Hasna Mwilima
“Lazima ifike mahala tuambiane ukweli, abiria wa mkoa wa Kigoma wanateremshwa wote wanaanza kauambiwa tuone uraia wako. Hali ya operation zisizo na ubinadamu hatuzitaki ndani ya Kigoma” –Hasna Mwilima
Onyo alilolitoa Waziri mkuu Majaliwa kwa TRA