Leo Desember 4, 2017 Rais John Magufuli amekutana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bella Bird, Ikulu DSM na kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo.
Bird ameeleza kuwa benki hiyo imejipanga kuendelea kutoa mikopo nafuu kwa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
Amebainisha maeneo ya kipaumbele kuwa ni miundombinu hususani barabara na reli, kuongeza uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na elimu.
Mengine ni pamoja na upatikanaji wa maji, usimamizi bora wa ardhi, mawasiliano, huduma za fedha jumuishi, vituo vya pamoja vya Serikali na kusaidia familia masikini.
Ulipitwa na hii? TANZANIA YAKOPESHWA: BENKI YA DUNIA YAIPA BILIONI 340