Bilionea mkubwa nchini Urusi Kirill Shamalov anaripotiwa kupoteza nusu ya utajiri wake siku za hivi karibuni kipindi ambacho kumesambaa taarifa za kuachana rasmi na mkewe Katerina Tikhonova ambaye ni mtoto wa Rais wa nchini hiyo Vladmir Putin.
Inasemekana kuwa mkwe huyo wa Rais Putin ambaye anatajwa kuwa bilionea mdogo nchini humo amevuliwa vyeo pamoja na nusu ya utajiri wake kuchukuliwa ikiwa kama adhabu baada ya kuachana na mke wake ambaye walikuwa wameoana tangu mwaka 2013.
Inaripotiwa kuwa tayari Shamalov yuko kwenye uhusiano mpya wa kimapenzi na mwanamke aitwaye Zhanna Volkova mwenye asili ya Urusi anayeishi London baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook December 2017 ujumbe unaosema ‘Nakupenda’ ukimlenga mpenzi wake mpya huyo.
Hospitali ya Bugando Mwanza wamepata kifaa cha CT-SCAN, Kwa mara ya kwanza.
Mbowe azindua Kampeni Siha, Mgombea Elvis Mosi aongea