Mtanzania ‘Chef’ Fred Uisso amechaguliwa kushiriki kwenye fainali za mashindano ya World Food Championships 2016 zinazotarajiwa kufanyika Novemba 8-15, baada ya kufanya vizuri katika upishi wa nyama ‘Best Stake Chef’ mapema mwaka huu.
Chef Uisso ambaye ni mpishi mwandamizi katika mgahawa wa Afrikand uliopo Kinondoni, anakuwa Mwafrika wa kwanza kupata nafasi ya kushiriki katika mashindano hayo, ambayo yamefanyika kwa kipindi cha miaka 15 mfululizo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001 baada ya kufadhiliwa na Red Gold Tanzania.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Chef Uisso alisema amepata nafasi ya kwenda kushiriki mashindano hayo mwezi ujao Alabama States nchini Marekani baada ya kushiriki kupitia mtandaoni mara kadhaa.
‘Walinitambua kupitia kazi zangu ambazo nilizifanya mtandaoni, katika dunia nzima ambao tuliingia katika mtandao huo tulikuwa zaidi ya watu 3700 ambao kila mmoja alionyesha uwezo wake wa kupika vyakula mbalimbali, nilirekodi na kuweka katika mtandao huo na majaji watatuchagua washindi 100 katika kila kipengere’
Alisema baada ya kuchaguliwa 100 katika vipengere 9, jumla ya washiriki 900 walipatikana na kuchujwa hadi kufikia 50. Baadaye walipewa kazi nyingine na kisha kuchujwa mpaka kufikia 21 ambao ndiyo walioingia fainali.
Unaweza ukabonyeza play kumtazama mtanzania aliyechaguliwa kushiriki fainali za Worlsd Food Championships 2016
ULIIKOSA MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU KUHUSU MAMOBI YA MBOWE KURUDISHWA KWENYE JENGO NHC BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA