July 5, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilihutubia Bunge kabla ya kuliahirisha hadi September 5, 2017 ambapo katika hotuba yake hiyo aligusia issue mbalimbali ikiwemo ya wanafunzi wanaopewa mimba wakiwa shuleni.
Katika Hotuba hiyo Waziri Mkuu Majaliwa amegusia mambo mbalimbali ikiwemo Elimu hasa ya watoto wenye mahitaji maalum ambao Serikali imewapa kipaumbele.
“Serikali imeendelea kutafuta suluhu ya kutatua changamoto za kujifunzia zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji maalum…hivi karibuni Serikali imenunua vifaa kwa ajili ya wanafunzi wasioona na wenye baki ya usikivu na kuvisambaza kwenye shule 213 za Msingi na 22 za Sekondari.”
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa ameelezea pia msimamo wa Serikali kuhusu wanafunzi wa kike wenye ujauzito kurudi shuleni baada ya kujifungua akisema ni msimamo wa kisheria wenye lengo la kulinda maadili.
“Msimamo wa Serikali wa kutoruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo katika mfumo rasmi wa elimu ni kwa mujibu wa sheria na wala sio utaratibu mpya kama inavyopotoshwa na baadhi ya Wanaharakati. Msimamo huo wa kisheria unalenga kuwafanya watoto wa kike wajishughulishe na masomo yao badala ya kushiriki kwenye vitendo vya ukiukwaji wa maadili.” – Waziri Mkuu Majaliwa.
VIDEO hii ina HOTUBA yote ambayo Waziri Mkuu aliitoa kabla ya kuahirisha Bunge hadi September mwaka huu.