Kampuni ya Ecobank Tanzania ambayo ni mshirika wa Ecobank Group, kikundi cha benki kinachoongoza barani Afrika, kwa kushirikiana na Shule Direct wametoa ada ya kujiunga na Shule Direct mtandaoni kwa muda wa mwaka mmoja na tablet 13 kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi na kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule, maabara ya computer kwa shule ya Sekondari Mugabe iliyopo Sinza Dar es Salaam katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya Siku ya Ecobank inayofanyika kila mwaka.
‘Siku ya Ecobank’ ni tukio kubwa la ushirika na uwajibikaji kwenye jamii ambapo Ecobank na wafanyakazi wake kurudisha fadhila zao kwenye jamii.
Mchango huu unaendana na uzinduzi wa kampeni mpya ya miaka mitatu ya ‘Siku ya Ecobank’ iliyozinduliwa na washirika 33 wa Ecobank.
Kauli mbiu ya kampeni hii ni ‘Kubadilisha Afrika Kupitia Elimu’ Mwaka wa kwanza wa kampeni utaangazia elimu ya kidijitali na kutengeneza fursa kwa watoto na vijana ili wapate ujuzi wa kidijitali wanaohitaji kwaajili ya kujitengenezea kesho yao Ecobank, inataka kujenga maabara 33 za TEHAMA kama sehemu ya mpango wake wa miaka 10 ya Siku ya Ecobank.
Charles Asiedu, Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania, alisema: “Idadi ya watu Tanzania inatabiriwa kufikia milioni 129.4 ifikapo 2050 na ni muhimu kuwapa vijana wetu ujuzi bora zaidi ambao utawaweka kwa ajili ya ubora wa kesho yao.
Tuko katika kipindi cha kutekeleza maendeleo ya haraka kupitia teknolojia huku ujuzi wa kidijitali ukihitajika na waajiri. Tunajivunia kuwa sehemu ya simulizi mpya ya elimu ya kidijitali nchini Tanzania kupitia mchango huu. Ningependa kuwashukuru washirika wetu waliofanikisha siku hii kwa vijana wetu.”Siku ya Ecobank imesaidia na kuendeleza mambo mbalimbali muhimu kila mwaka tangu 2013.
Haya yamekuwa Elimu kwa vijana barani Afrika (2013); Kuzuia na kudhibiti Malaria (2014); Kila mtoto wa Africa anastahili maisha bora ya baadae (2015); Elimu ya TEHAMA shuleni na kuboresha afya ya uzazi (2016); usimamizi wa maji salama (2017); Vituo vya watoto yatima (2018); Saratani (2019); Kisukari (2020); Afya ya akili (2021) na ujuzi wa kifedha na ushirikishwaji wa kifedha (2022).