Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) imesimamisha uanachama wa Niger baada ya serikali kuu ya kijeshi kukataa kumrejesha madarakani Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum.
Bazoum alipinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi mwezi Julai.
Ecowas ilisema katika taarifa Alhamisi kwamba mkutano wa hivi karibuni wa viongozi wake nchini Nigeria “ulitambua” kwamba serikali ya Bw Bazoum “ilipinduliwa kikamilifu katika mapinduzi ya kijeshi”.
Imeisimamisha Niger katika vyombo vya kufanya maamuzi vya Ecowas hadi “utaratibu wa kikatiba utakapo rejeshwa nchini humo”.
Hali ya nchini Niger awali ilichukuliwa na Ecowas kama jaribio la mapinduzi, na hivyo kusababisha kuchelewa kusimamisha uanachama wa nchi hiyo.