Maofisa wa ulinzi kutoka katika Jumuiya ya Ecowas, wanatarajiwa kukutana leo Jumatano mjini Abuja nchini Nigeria kujadili mapinduzi ya kijeshi yaliotokea nchini Niger wiki iliyopita.
Awali Ecowas ilikuwa imewapa wanajeshi waliohusika na mapinduzi hayo kipindi cha wiki moja kurejesha utawala wa rais Mohamed Bazoum na kutishia kutumia nguvu iwapo hilo halitazingatiwa.
Tayari nchi ya umoja na ulaya ikiwemo Ufaransa zimeanza kuwaondoa raia wake nchini Niger, Paris ikiwasafirisha raia wake 250 kwa kutumia ndege tatu.
Hatua ya kuwaondoa raia hayo wa kigeni ikija kufuatia hatua ya waandamanaji kuvamia ubalozi wa Ufaransa siku ya Jumapili.
Italia nayo pia ikiwa imechukua hatua kama ya Ufaransa na nchi zengine za EU, Marekani nayo pia ikiwa imewaondoa raia wake.
Utawala wa kijeshi umetangaza kufunguliwa tena kwa mipaka yake na mataifa ya Algeria, Burkina Faso, Libya, Mali na Chad.
Ufaransa imeanza kuwahamisha mamia ya raia wa Ufaransa na Ulaya kutoka Niger, siku chache baada ya Rais Mohamed Bazoum kupinduliwa na walinzi wake wa rais.
Safari ya kwanza ya ndege tatu za kuwahamisha raia wa Ufaransa na Ulaya kutoka Niger iliondolewa Jumanne jioni.
Ufaransa, Italia na Uhispania zote zilikuwa zimetangaza kuhama kutoka Niger kwa raia wao na raia wengine wa Uropa.