Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ameonyesha kukerwa sana na uzembe uliofanywa na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa kwa kusasua ujenzi wa kituo cha Afya Mikumi licha ya kupokea fedha tangu mwishoni mwa mwezi June 2018.
Katika ziara hiyo ya kushtukiza watendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilosa asubuhi ya leo na kupeleka mchanga zaidi ya Maroli sita pamoja na fundi aliyekuwa akichanganya mchanga huo ili ionekane kazi inaendelea lakini waziri Jafo aligundua janja hiyo na kutoa maagizo mazito kwa Uongozi wa Halmashauri hiyo. ‘ Niwatake Mkurugenzi wa Kilosa, Mweka Hazina, Mkanga Mkuu wa Wilaya, Afisa Mipango pamoja na Mhandisi kuwasilisha barua zenu haraka sana Ofisi ya Rais Tamisemi za kujieleza kwanini msichukuliwe hatua kutokana na uzembe mlioufanya katika kituo hiki’ aliagiza Jafo.
Aliongeza kuwa Mpaka sasa kituo hikiwapo katika hatua ya msingi wakati wenzao wa maeneo mengine waliopewa fedha wakati mmoja wakiwa katika hatua za umaliziaji.
Ziara hiyo ya waziri Jafo Mkoani Morogoro amefanikiwa kutembelea ujenzi wa kituo cha afya Mikumi, ujenzi wa kituo cha afya Kidodi, pamoja na kutembelea eneo la Luhembe ambapo patajengwa daraja kubwa litakalo gharimu zaidi ya shilingi milioni mia nane.