Jumamosi ya April 29 2017 mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Azam Sports Federation Cup msimu wa 2016/17 ilichezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa kuzikutanisha timu za Simba dhidi ya Azam FC, huo ukiwa ni mchezo wa tatu kwa timu hizo kukutana kwa mwaka 2017.
Simba leo imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza dhidi ya Azam FC kwa mwaka 2017 baada ya kupoteza michezo yao miwili kati ya mitatu waliyocheza dhidi ya Azam FC kwa mwaka 2017, Simba leo imefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Mohamed Ibrahim dakika ya 48 kwa kutumia vyema pasi kutoka kwa Laudit Mavugo.
Simba sasa inaingia fainali ya Kombe la FA na itakuwa inasubiri mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya kesho kati ya Yanga dhidi ya Mbao FC mchezo unaochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, kama utakuwa unakumbuka vizuri Simba alipoteza mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC January 13 kwa goli 1-0.
Mchezo wao wa pili kupoteza ukawa uwanja wa Taifa Dar es Salaam January 28 mchezo wa marudiano kwa goli 1-0, kabla ya mchezo wa leo Simba iliifunga Azam FC kwa mara ya mwisho ilikuwa Septemba 17 2016 katika uwanja wa Uhuru mchezo wa round ya kwanza wa Ligi Kuu Vodacom msimu wa 2016/2017.
VIDEO: Adhabu aliyopewa Haji Manara wa Simba na kamati ya nidhamu ya TFF