July 15 2016 ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ‘Muhimbili‘ imeweza kufanya matibabu ya kumuwekea mgonjwa kifaa cha kusaidia moyo kufanya kazi zake kwa mtoto wa miaka mitano, kifaa hicho kinaitwa pacemaker operation hii ni ya kwanza kwa Tanzania kufanyika kwa mtoto.
Mtoto huyu alikuwa na ugonjwa unaoitwa concenital heart block uliokuwa unasababisha mapigo ya moyo kuwa chini sana na kumsababisha kushindwa kumudu maisha ya kawaida kwa umri wake.
Uongozi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ‘Muhimbili’ wamewataka watanzania watambue uwepo wa huduma hiyo katika taasisi na kwamba kwa wale ambao wanashida juu ya mapigo ya moyo, wanaweza kwenda kwenye taasisi na kufuatilia matibabu.
ULIKOSA HII YA WAZIRI MWALIMU KUJA NA MAAMUZI HAYA KUHUSU UTOAJI CHAKULA MUHIMBILI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI