Kurusha Bra’s jukwaani wakati wa matamasha ya Drake kumekuwa kukienea kwenye mitandao ya kijamii, lakini wakati wa ziara yake mjini Los Angeles rapper huyo alibadili mambo kidogo na kuwaambia mashabiki wasirushe sidiria zao jukwaani.
“Haya sikiliza. Siwezi kuongelea bra’s usiku wa leo hapa LA kwa sababu mwanangu yuko kwenye show kwa mara ya kwanza kabisa,hivyo tafadhali weka sidiria zako usiwe unazitupa hapa au chochote.” aliandika kwenye insta story yake.
Awali mtoto wake Adonis alikuwa kwenye jengo hilo na Drake hata akamwimbia moja ya nyimbo zake wakati wa onyesho hilo.
Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wanamchukulia nyota huyo kama “baba wa mwaka baada ya tukio hilo”
#Drake had to go braless at his recent concert in LA due to his 5-year old son Adonis being in the building. He asked fans to chill on throwing bras after scooting some off the stage w/ his foot. Overall, the show had no bra action and was still great. (🎥 tiktok: therealkduece) pic.twitter.com/hqlDRZSA98
— theJasmineBRAND (@thejasminebrand) August 13, 2023