Kwenye ile time ya maswali na majibu ndani ya Kikao cha Bunge la Tanzania, Dodoma leo kulikuwa na maswali ambayo yamegusia agizo la Rais Magufuli kuhusu elimu kutolewa bure kwa shule za msingi mpaka kidato cha nne.
Maswali yakaulizwa na hapa ni sehemu ya majibu kuhusu utaratibu mzima wa elimu hiyo mpaka mabilioni ya Rais Magufuli yanavyofikishwa shuleni.
‘Serikali imeamua kuanzia January 2016 fedha za ada na michango kwa sasa zitalipwa na Serikali… Bilioni 131 tayari zimetengwa kwa ajili ya chakula, ada na mitihani na zitapelekwa moja kwa moja shuleni kutoka hazina… Bilioni 18 tayari zimepelekwa kwa January 2016 mashuleni.’- Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jaffo.
‘Wazazi wengi walishindwa kulipia gharama za kujiunga shule za msingi na Sekondari… kwa sasa imefikia hatua hata madarasa hayatoshi, Serikali imefanya jitihada kubwa na changamoto ndogondogo zitaboreshwa mpango uende vizuri… Hatutarajii mwalimu azuie mwanafunzi asiende shule kwa sababu amezusha mchango wake mwenyewe, hii elimu ni bure.’- Naibu Waziri, Selemani Jaffo.
‘Serikali itapeleka kila mwezi kwa ajili ya shule za msingi na sekondari… uwezekano wa kuendesha elimu upo pamoja na changamoto zinazoonekana.’- Waziri George Simbachawene.
‘Kutokana na elimu bure, tulipotegemea watajiandikisha watoto 80 darasa la kwanza wamejiandikisha 240, tulipotaka wajiandikishe watoto 180 wamejiandikisha karibu 700 na hiyo ni Dar pekeyake… yapo maeneo uwezekano wa kupokea watoto ni mgumu kwa sababu wazazi wameona mpango huu unawasaidia, tupingane katika mengine lakini kwenye jambo zuri tutiane moyo kama Watanzania.’-Waziri Simbachawene.
Maswali na majibu kwa Wabunge hao na Mawaziri yako kwenye sauti hii mtu wangu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE