Elon Musk, Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla na SpaceX, ameelezea matumaini kuhusu mustakabali wa Neuralink, akitabiri kupitishwa kwa chip yake ya ubongo ndani ya miaka kumi ijayo.
Hii inafuatia maendeleo ya kutia moyo na mpokeaji wa pili wa kipandikizi, ambaye anaripotiwa kupitia maboresho makubwa katika uwezo wake wa kuingiliana na vifaa vya kidijitali.
Kampuni hiyo iliarifu kwamba mwezi uliopita, Alex, mshiriki wa pili katika ‘PRIME Study’, alipokea kipandikizi chake cha Neuralink.
“Upasuaji, uliofanywa katika Taasisi ya Neurological Barrow, ulikwenda vizuri – Alex aliruhusiwa siku iliyofuata, na sasa amepata ahueni ,” ilisema Neuralink.
Akiwa na chip hiyo, amekuwa akiboresha uwezo wake wa kucheza michezo ya video [games] na kuanza kujifunza jinsi ya kutumia programu inayosaidiwa na kompyuta (CAD) kubuni vitu vya 3D.
“Hii inaashiria hatua nyingine muhimu kuelekea kutoa kiolesura cha utendakazi wa hali ya juu ambacho kitaimarisha udhibiti wa vifaa vya kidijitali kwa watu wenye matatizo ili kusaidia kurejesha uhuru wao,” kampuni hiyo ilibainisha.
“Tunatumai kuwa baada ya muda, programu hii kusaidia watu wengi kuunda kile wanachokipenda na utaalamu binafsi, na tunafurahi kufanya kazi na watu zaidi ili kuwasaidia kuungana tena na matamanio yao,” kampuni hiyo ilisema.