Alitangaza habari hizo kwenye mtandao wa kijamii, alioununua mwaka jana kwa $44bn (£35.2bn). Bw Musk hakumtaja Mkuu mpya wa tovuti hiyo lakini alisema “yeye” angeanza baada ya wiki sita, ambapo atakuwa Mwenyekiti Mtendaji na afisa mkuu wa teknolojia.
Amekuwa chini ya shinikizo la kutaja mtu mwingine kuongoza kampuni na kuzingatia biashara zake nyingine. Mwaka jana, baada ya watumiaji wa Twitter kumpigia kura ya kumtaka aachie ngazi katika kura ya maoni mtandaoni, alisema: “Hakuna anayetaka kazi hiyo ambaye anaweza kuIweka Twitter hai.”
Hata hivyo, ijapokuwa Bw Musk alikuwa amesema angekabidhi majukumu, haikuwa wazi ni lini au hata ikiwa ingefanyika.
Hisa za Tesla ziliongezeka baada ya tangazo. Hapo awali Bw Musk alishtumiwa na wenye hisa kwa kuitelekeza Tesla baada ya kuchukua Twitter na kuharibu chapa ya kampuni hiyo ya magari.
Uamuzi wa Musk wa kuteua Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Twitter huenda ukawafurahisha wawekezaji wa Tesla, ambao wamekuwa na wasiwasi kwamba muda wa Musk kwenye Twitter unamwondolea nafasi yake kama Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla. Kufuatia habari kwamba alipata mbadala wa jukumu hilo, hisa za Tesla ziliongezeka.
Hivi majuzi Musk alibadilisha jina la Twitter Inc. kuwa X Corp. Kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuunda kile anachokiita “X, programu ya kila kitu.”