Wapenzi wawili, Lee Hops na Hayley McClory waliokamatwa wakifanya mapenzi kwenye choo cha pub moja mitaa ya Durman, Uingereza wamepandishwa kizimbani kusomewa mashtaka ya makosa mbalimbali.
Siku ya tukio mhudumu mmoja wa aliwakuta na kutoa na taarifa Polisi ambao waliwaamuru watoke lakini walikataa hadi walipotumia gesi ya pilipili ili kuwatoa wawili hao na kuwakamata katika choo cha pub ya Wetherspoons.
Wanandoa hao wanashtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ya kupinga amri ya Polisi, kutoa maneno ya vitisho na matusi na kosa la kumshambulia Polisi na kuchana koti lake.
Hata hivyo walikana mashtaka hayo huku wakilalamika kwamba sheria ilikiukwa kwa wao kupuliziwa gesi hiyo wakati wa kukamatwa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook