Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki Dr. Augustine Mahiga ameeleza kuwa Uingereza ni moja ya nchi tano muhimu duniani zinazowekeza kwa wingi Tanzanai kwa ajili ya maendeleo katika sekta binafsi, viwanda na biashara.
Akizungumza na Wanahabari wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Stewart Rory, Waziri Mahiga amesema Uingereza wamekuwa mstari wa mbele kusaidia sekta ya elimu huku naye Waziri Rory akisema nchi yake imejipanga na huwa inatenga fungu maalumu kwa ajili kuinua kiwango cha elimu katika nchi ya Tanzania.
>>>”Serikali ya Uingereza ina furaha kushirikiana na Serikali ya Tanzania hasa katika sekta ya elimu, kuboresha elimu kwa kutoa Pound Milioni 140 ikiwa ni moja ya miradi mikubwa duniani ya kuboresha miundombinu ya maji na usafi wa mazingira.” – Waziri Rory.
“KUNA WATU WANA KIBURI…” – WAZIRI MWIJAGE