Nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria na golikipa wa klabu ya Lille ya Ufaransa Vincent Enyeama, siku ya Septemba 2 ameingia katika headlines na shirikisho la mpira wa miguu Nigeria (NFF). Enyeama anaingia katika headlines baada ya kujitoa katika timu ya taifa kwa matatizo anayodai ni ya kifamilia.
Kwa mujibu wa mtandao wa ripples.com nahodha huyo wa timu Nigeria, alituma meseji kwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Sunday Oliseh na kueleza uamuzi wake kwa nini amejiengue katika timu yake ya taifa kwa sasa na hawezi kuwepo katika mechi zote muhimu.
Enyeama anaeleza kuwa hawezi kuwepo, ana matatizo ya kifamilia ambayo yanahitaji uangalizi wake hivyo hawezi kuwepo, taarifa hizi zinakuja ikiwa ni siku chache zimebaki kabla ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, kuja Tanzania kucheza mechi na Taifa Stars Septemba 5 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Tamko la NFF kuhusu uamuzi wa Enyeama ni kuwa, sababu alizozitoa sio za msingi za kushindwa kuiwakilisha nchi yake katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2017. Ikumbukwe kuwa Enyeama aliitwa na Sunday Oliseh katika timu ya taifa ya Nigeria baada ya kuwa amefungiwa na NFF kutokana na kauli yake aliyowahi kuitoa kuhusu hali ya usalama Kaduna.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos